"NIMEBAKWA NA BOSI WANGU WA KIKE....NAOMBENI USHAURI WENU JAMANI".....MDAU
Gumzo skendo
Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa na hivyo nimeamua niwe muwazi ili niweze kusaidiwa.Sihitaji msaada wa kifedha, bali nahitaji ushauri tu.
Ndugu zangu mwenzenu juzi jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu baada ya kubakwa na mama mke wa mtu.
Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika sehemu moja ya starehe .
Mimi ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu.
Mume wake siyo mtu wa kushinda sana nyumbani.Ni mfanyabiashara na mara nyingi huwa nje ya nchi kibiashara. Nyumba yao ina geti kubwa na mlinzi mmoja.
Baada ya kumpeleka huko mapumzikoni, saa tano usiku alinipigia simu nikamchukue ili nimrudishe nyumbani. Nilimkuta akiwa amelewa sana, hivyo nikamkokota mpaka ndani ya gari tukaondoka.
Nyumbani tulikuta mwanae mdogo na house girl wamelala hivyo akaniomba nimpeleke chumbani kwake kwa madai kwamba alikuwa hawezi kutembea kwa sababu alizidisha pombe.
Nilimvuta mpaka chumbani kwake maana sikuwa na jinsi ya kukataa.Cha ajabu nilipomfikisha chumbani yule mama alipata nguvu akafunga mlango.
Alisimama pale mlangoni na kuanza kuvua nguo zake.Nilipojaribu kumvuta ili nitoke, yule mama alitishia kupiga kelele.Akanambia nitulie tulale, vinginevyo atapiga kelele kwamba nataka kumbaka.
Nikifikiria getini kuna mlinzi na nipo ndani ya chumba cha bosi wangu kiasi kwamba mlinzi akija ni lazima aamini kwamba nilikuwa nataka kumbaka..
Akili ya haraka haraka ilinituma nimkubalie tu, lakini nikakumbuka pia sina hata kipande cha kondom.
Jmani naomba niishe hapo maana nashindwa kuendelea kuelezea.Kwa kifupi ni kwamba nilifanya mapenzi na yule mama bila kinga yoyote.
Mlinzi alijua kila kitu tulichokifanya maana niliondoka asubuhi.Siwezi kuendelea na kazi tena maana mumewe akirudi ni lazima aambiwe kila kitu..
Kinachoniuma ni kwamba kazi nimeipoteza na huenda afya yangu nayo ikawa imeingia dosari.Tangu juzi sijafanya mapenzi na mke wangu.Nasubiri miezi mitatu ipite ili nikapime.
Lakini namwelezaje mke wangu kwa kipindi chote hicho ili anielewe.Na mimi kama mumewe naanzaje kumweleza kwamba nimebakwa? Ndoa yangu itakuwaje?
Naomba msaada wa ushauri toka kwenu na kwa wasomaji wenu.
Ni mimi
Jose.
HABARI MPYA

Na Happiness Katabazi — MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetengua adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa na Mahakam...
.jpg)
Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa na hivyo nimeamua niwe muwazi ili niweze kusaidiwa.Sihitaji msaada ...

ZITTO KABWE KUFUNGA SAFARI YA KWENDA USWISS NA UINGEREZA KUFUATILIA MABILIONI YALIYOFICHWA HUKO...!!
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Deokrasia na Maendeleo (Chadema) Ndg. Zuberi Zitto Kabwe. Shirika la Kimataifa la M...

Vitendo vya ukatili wa kijinsia viko vingi na vya aina tofauti tofauti. Kuna wanawake wengine wanafanyiwa vitendo hivi bila kujua kuwa ni kinyume...

Hawa ni vijana wa kitanzania 11 ambao walikamatwa na jeshi la polisi Mtwara baada ya ...

HATUA ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakaz...

Siku chache baada ya kuanzisha ukaguzi wa magari na watu wanaoingia katika maduka ya Mlimani City, ukaguzi huo sasa umesitishwa. ...

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘ Maya ’ amefunguka kuwa wale waliozusha kuwa amechumbiwa, watasubiri sana kwani suala la ndoa kwake bado h...

INAUMA sana! Mtuhumiwa wa unyongaji wa mwanamke aliyeelezwa kuwa ni mke wa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Ana Mbago amenaswa kufuatia tukio...
ANGALIA VIDEO HAPO CHINI.......

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood ambaye ndiye mmiliki wa Kituo cha Abood Media alipokuwa akifanya kazi marehemu Nyaisangah akimpa mkono...

Wakati ikisubiriwa ripoti ya uchunguzi wa Tume Maalumu iliyoundwa kwa Azimio la Bunge kuchunguza kashfa ya vigogo walioficha Sh323.4 bilioni katika...
Popular Posts
- KATIKA hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amenaswa akiwa ametinga khanga moja na kuwaacha watu midomo wazi...
- Mwanaume aliyetambulishwa kwa jina la Mchungaji Mayanga amewashangaza waumini baada ya kudai kanisani kuwa yeye ndiye aliyewaua mastaa wawi...
- WABONGO walisema nabii asifiwi kwao, hicho ndicho kilichomtokea msanii wa muziki wa bongo fleva Nassib Abdul, maarufu kwa jina la Diamond ...
- Julius Nyaisanga a.k.a Anko J (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkongwe Mwenzie,Aboubakar Liongo HABARI zilizotufikia ...
- Wema Sepetu mwenyewe anajua kwamba watu wengi wanafikiri yeye anawaza kuwa na Diamond hivi sasa, lakini ametoa majibu ya hayo mawazo k...
- Takribani week sasa habari kubwa kuhusu mastaa Bongo ni story ya Diamond na Wema ,kurudiana ambapo habari hizo bado ni tata kutokan...
- Baadhi ya ndugu wa marehemu Anthery Mushi wakilia kwa uchungu walipokuwa wakitoa salamu za mwisho Muhimbili leo. Baadhi ya ndugu,...
- Kutana na mwendelezo wa mwanamama flora Lymo ni mtanzania anayeishi nje ya nchi ambaye yuko kwenye "SERIES" ya kupiga a pic...
- 1. DIAMOND KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU TIMU NZIMA YA THECHOICE ILIWEZA KUFANYA UTAFITI KWA KINA JUU YA KUFAHAMU WANAMUZIKI WA BONGO ...
- MSANII wa filamu nchini Tanzania Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la (Lulu) ameonyesha kufurahishwa na tukio la wanaume wengi wenye ...