Jumatatu, 21 Oktoba 2013


"NIMEBAKWA NA BOSI WANGU WA KIKE....NAOMBENI USHAURI WENU JAMANI".....MDAU




Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa  na hivyo nimeamua niwe  muwazi  ili  niweze  kusaidiwa.Sihitaji  msaada  wa  kifedha, bali  nahitaji  ushauri  tu.

Ndugu zangu mwenzenu juzi   jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu  baada  ya  kubakwa  na  mama  mke  wa  mtu. 

Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika  sehemu moja ya starehe .

Mimi ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu.

Mume  wake  siyo  mtu  wa  kushinda  sana  nyumbani.Ni  mfanyabiashara  na  mara  nyingi  huwa  nje  ya  nchi  kibiashara. Nyumba  yao  ina  geti  kubwa  na  mlinzi  mmoja.

Baada  ya  kumpeleka  huko  mapumzikoni, saa tano  usiku  alinipigia  simu  nikamchukue  ili  nimrudishe  nyumbani. Nilimkuta  akiwa  amelewa  sana, hivyo  nikamkokota  mpaka  ndani ya  gari  tukaondoka.

Nyumbani  tulikuta  mwanae  mdogo  na  house girl  wamelala  hivyo  akaniomba  nimpeleke  chumbani  kwake  kwa  madai  kwamba  alikuwa  hawezi  kutembea  kwa  sababu  alizidisha  pombe.

Nilimvuta  mpaka  chumbani  kwake  maana  sikuwa  na  jinsi  ya  kukataa.Cha  ajabu  nilipomfikisha  chumbani yule  mama  alipata  nguvu akafunga  mlango.

Alisimama  pale  mlangoni  na  kuanza  kuvua  nguo  zake.Nilipojaribu  kumvuta  ili  nitoke, yule  mama  alitishia  kupiga  kelele.Akanambia  nitulie  tulale, vinginevyo  atapiga  kelele  kwamba  nataka  kumbaka.

Nikifikiria  getini  kuna  mlinzi  na  nipo  ndani  ya  chumba  cha  bosi wangu  kiasi  kwamba  mlinzi  akija  ni  lazima  aamini  kwamba  nilikuwa  nataka  kumbaka..

Akili  ya  haraka  haraka  ilinituma  nimkubalie  tu, lakini  nikakumbuka  pia  sina  hata  kipande  cha kondom.

Jmani naomba  niishe  hapo  maana  nashindwa  kuendelea  kuelezea.Kwa  kifupi  ni  kwamba  nilifanya  mapenzi na  yule  mama  bila  kinga  yoyote. 

Mlinzi  alijua  kila  kitu  tulichokifanya  maana  niliondoka  asubuhi.Siwezi  kuendelea  na  kazi  tena  maana  mumewe  akirudi  ni  lazima  aambiwe  kila  kitu..

Kinachoniuma  ni  kwamba  kazi  nimeipoteza  na  huenda  afya yangu nayo  ikawa  imeingia  dosari.Tangu  juzi  sijafanya  mapenzi  na  mke  wangu.Nasubiri  miezi  mitatu  ipite  ili  nikapime. 

Lakini  namwelezaje mke  wangu  kwa  kipindi  chote  hicho  ili  anielewe.Na  mimi  kama  mumewe  naanzaje  kumweleza  kwamba  nimebakwa?  Ndoa  yangu  itakuwaje?

Naomba  msaada  wa  ushauri  toka  kwenu  na  kwa  wasomaji  wenu.

Ni  mimi 
Jose.

LIKE UKURASA WETU HAPA..!!


 

HAWA NDO WANAMUZIKI 5 MATAJIRI TANZANIA UTOKANAO NA MUZIKI WA BONGO FLEVA ...


1. DIAMOND 
 
KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU TIMU NZIMA YA THECHOICE ILIWEZA KUFANYA UTAFITI KWA KINA JUU YA KUFAHAMU WANAMUZIKI WA BONGO FLEVA WENYE MAFANIKIO ZAIDI KUTOKANA NA MUZIKI HUO,TIMU YA THECHOICE IMEWEZA PATA WANAMUZIKI WATANO WENYE MAFANIKIO ZAIDI KUTOKANA NA MUZIKI HUO.
NI MSANII ALIYE LETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MUZIKI HASAHASA KATIKA SHOW ZA STEJINI YAANI LIVE PERFORMANCE .NI MSANII ANAYE LIPWA PESA NYINGI KWA SASA TANZANIA KWA SHOW MOJA ANAYO FANYA.PIA NI MSANII MWENYE SHOW NYINGI KWA MWEZI KULIKO WOTE,.HII IMECHANGIA KUWEZA KUPATA PESA NYINGI KATIKA MDA MFUPI.ANAMILIKI NYUMBA KADHAA,VIWANJA,MAGARI,MADUKA.
DIAMOND


GARI ANAYO MILIKI YENYE THAMANI YA TSH.MIL 60

GARI ALIYO KUWA ANATEMBELEA MWANZO


2. LADY JAY DEE
NI MSANII MWENYE HESHIMA SANA TANZANIA KUTOKANA NA KUJIHESHIMU KWAKE,KAPATA MAFANIKIO SANA KATIKA KAZI ZAKE ZA MUZIKI NA KUWEZA KUWA MFANO WA KUIGWA KWA WASANII WENGINE.KWANI UCHAPA KAZI WAKE NDO SABABU YA MAFANIKIO YAKE KIMAISHA.
MALI ANAZOMILIKI NI PAMOJA NA -GARI AINA YA MURANO THAMANI YA 
TSH.MIL 45, BASI AINA YA COSTA TSH.MIL.30, PRADO, NYUMBA NZURI YA KISASA,PAMOJA NA MGAHAWA WA NYUMBANI LONGE WENYE THAMANI YA ZAIDI YA TSH.MIL.150 PIA ALIANZISHA MAJI YAKE YA JAY DEE AMBAYO BAADAYE YALIZUIWA.


NYUMBANI LONGE KWA NDANI

NYUMBANI LONGE KWA NDANI

MAJI YA JAY DEE


NYUMBA YA KISASA ANAYOISHI
BASI KWA AJILI YA BAND YAKE YA MACHOZI BAND
3.AY
  AY NI MSANII MKIMNYA SANA NA HUWA HAWEKI MAMBO YAKE HADHARANI SANA HASAHASA YA MAISHA YAKE.LAKINI NI MSANII MWENYE PESA NYINGI KUTOKANA NA KUFANYA SHOW NYINGI ZA KIMATAIFA ZINAZO MPATIA PESA NYINGI.ANAMILIKI MAGARI,ANA DUKA LA NGUA,PIA ANA NGUO ZAKE MAALUMU ZENYE NEMBO YA JINA LAKE.

4.PROF J 
NGULI WA MUZIKI WA BONGO FLEVA TANZANIA,ANAFANYA SHOW NYINGI ZA NJE,NI MSANII AALIYE DUMU KWA MDA MREFU,ANAMILIKI NYUMBA YA KISASA YA ZAIDI YA TSH.MIL 100, ANAMILIKI GARI,MASHAMBA
PROF.J
NYUMBA YA PROF J
 
MBELE YA NYUMBA
Mwanalizombe Studios Ni Recording Lebel Inayomilikiwa na Rapper Profesa Jay, Studio ipo msasani na Ameamua kuipa Jina la Mwanalizomba kwasababu Jay Ni mtu wa Ruvuma na Mwanalizombe maana yake ni Mwana Ruvuma na kufanya hivyo ameonyesha mapenzi ya mkoa wake wa Ruvuma. Producer kwenye studio hii ni Duke Touchez. 
 Profesa ameshindwa kusema amewekeza kiasi gani cha fedha kwenye studio hio ila fahamu kuwa vifaa vilinunuliwa kwa wakati tofauti na ni vifaa vya hali ya juu sana.
AINA YA GARI ANAYO TEMBELEA
 
 
KWA NDANI
 
KWA NJE   

Profesa Jay akinionyesha jina la Saloon yake iliyoko Msasani mbele karibu
 ni mitaa ilipokuwa Irish Pub
 5.JUMA NATURE

MSANII WA SIKU NYINGI KATIKA GEMU,KWA JINA JINGINE NI MKONGWE KATIKA MUZIKI WA TANZANIA HUU WA KIZAZI KIPYA,ANAMILIKI GARI,MASHAMBA,PIA  NI MFANYA BIASHARA ,ANAMILIKI NYUMBA,TUNASHUKURU KWA TIMU NZIMA YA THECHOICE KWA KUFANYA UTAFITI HUU.TUTAENDELEA KUWALETEA VITU VIZURI ZAIDI KILA SIKU NA ENDELEA KUWA NASI.

LIKE UKURASA WETU HAPA..!!